Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa amewataka watumishi 145 wa ajira mpya kufuata taratibu za kiutumishi na kushirikiana na watumishi pamoja na wananchi, hayo ameyasema leo April 9, 2025 alipokua akifungua mafunzo wa utumishi kwa watumishi hao.
Mhandisi Kawawa amewakaribisha watu.ishi hao katika Halmashauri ya Nachingwea na kuwasihi kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu na miongozo ya serikali inavyotaka, kufuata kanuni za utumoshi wa umma na kutumia busara katika kuhudumia wananchiambao ndio wateja wao.
Aidha, Mkuu wa Idara ya takwimu, Mipango na Ufuatilianji ndugu Joshua Mnyang'ali amesema kuwa Wilaya ya Nachingwea inategemea mapato yake kwa kiasi kikubwa katika Mazo ya biashara ambayo ni Korosho, ufuta na Mbaazi hivyo watumishi hao ni jukumu lao kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika mazao hayo kikamilifu na kuibua vyanzo vipya vya mapato.
Jumla ya watumishi wapya 145 wamepokelewa katika Halmashauri ya Nachingwea katika Idara za Utawala, Afya, Manunuzi, Tehama, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Fedha na Ujenzi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.