Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa amewataka wataalamu wanaosimamia miradi yote inayotekelezwa kuhakikisha miradi hiyo inazingatia ubora na kuikamilisha kwa wakati, hayo ameyasema leo April 9, 2025 alipofanya ziara ya kutembelea miradi.
Mhandisi Kawawa akiambatana na timu ya wataalam kutoka kutoka katika idara mbalimbali za Halmashauri hiyo amefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Naipingo, Ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Mtua wenye thamani ya Shilingi Milioni 560 katika kijiji cha Mtua na ujenzi wa Sekondari ya kata ya Nachingwea katika Kitongoji cha Kaloleni wenye thamani ya Shilingi milioni 560.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza wasimamizi wa miradi hiyo na kuwasisitiza kuzingatia viwango vya ubora na kumaliza kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma zitazotolewa katika miradi hiyo.
Aidha, Mhandisi Kawawa ametembelea Zahanati ya Kijiji cha Nchonda na Shule ya Msingi Nchonda na kuagiza uboreshwaji wa baadhi miundo mbinu katika taasisi hizo ili kuboresha upatikanaji wa huduma.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.