Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed H. Moyo amezindua rasmi maadhimisho ya wiki ya chanjo duniani ngazi ya wilaya kuanzia 24-30 april, 2023 ambapo amesisitiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wenye umri lengwa kupata chanjo katika vituo vilivyopangwa bure lengo kutokomeza magonjwa yanayo zuilika kwa chanjo ikiwemo ugonjwa wa surua na polio.
Mhe. Moyo. amesema katika maadhimisho hayo kuwa matarajio kuwafikia watoto 1871kwa mchanganuo ufuatao watoto 562 wenye umri chini ya miaka mitano ambao wamehasi chanjo, watoto 1127 waliopo katika ratiba ya chanjo na wasichana 182 wenye umri wa miaka 14 kwa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ambao wengi wao wapo shuleni.
Moyo, ametoa wito kwa viongozi wa vijiji, waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata, walimu na wadau mbalimbali kusimamia vema maadhimisho hayo kwa ufanisi mkubwa ili kufikia lengo la kila mlengwa kupata chanjo muhimu kwani kauli mbiu inasema "Tuwafikie watoto kwa chanjo " ikiwa imebeba ujumbe "Jamii iliyopata chanjo, jamii yenye afya "
Aidha, Mhe. Moyo amemalizia kwa msisitizo wa kuihasa jamii kuwa mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwa maisha yake na kwa jamii inayomzunguka kwani anaweza kuambukizwa au kuambukiza wengine ugonjwa kwa kutokuwa na kinga. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anakuwa mlinzi wa mwenzake.
#tukovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.