Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Mohamed Hassan Moyo amewasihi wachimbaji wadogo katika mgodi wa Kiegei kuhakikisha Mercury wanaotumia hafiki kwenye kingo za mto mbwemkuru kwani hathari za mekyuli ni kubwa sana kwa binadamu. Mhe Moyo ameyasema hayo June 13, 2023 alipokuwa kwenye ziara ya kukagua hali ya uchafuzi wa mazingira ambayo imetokea kwenye mgodi wa Kiegei wilayani hapo.
Aidha, Mhe Moyo ametoa siku saba kwa afisa madini wa wilaya kuhakikisha wote wanaokamatishia mekyuli kwenye mto wanachukuliwa hatua.
Kwa mujibu wa ndugu Taison ambae ni mtaalamu wa mionzi katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea amesema kemikali ya Mercury inaweza kusababisha matatizo ya afya kama vile kuharibika kwa figo, matatizo katika mfumo wa upumuaji, matatizo katika mfumo wa fahamu, vipele na ugonjwa wa kutetemeka Pia, kwa wamama wajawazito inapelekea matatizo kwa watoto kama vile mgogo wazi na kicha maji.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.