kuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo leo May 28, 2024 amefungua rasmi program ya huduma za Madaktari bingwa, "Madaktari wa Mama Samia" Wilayani Nachingwea ambazo zitatolewa katika hospitali ya Nachingwea. Katika ufunguzi huo viongozi na wananchi mbalimbali wamejitokeza kushuhudia na kupata huduma.
Jumla ya Madaktari bingwa sita wamewasili Wilaya ya Nachingwea siku ya May 27, 2024. Huduma zitakazotolewa ni pamoja na huduma za upasuaji, ganzi na usingizi, matibabu ya ngozi, huduma za Afya kwa watoto, magonjwa ya ndani na magonjwa ya wanawake na uzazi. Huduma hizo zitatolewa na Madaktari hao kwa muda wa siku tano.
Mhe Moyo amesihi wananchi kwenda kupata huduma hizo kwa wale wenye matatzito na wawape taarifa na wakazi wengine ambao hawajahudhuria. Pia, amesema "kumuona Daktari bingwa ni Bure" na malipo ni kwa huduma zingine kama dawa.
Akizungumza na wananchi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa ametoa shukurani za dhati na kumpongeza Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapa wananchi huduma Bora za Afya, pia amewasihi wakazi wa Nachingwea kutumia fursa hiyo kupata huduma za Madaktari hao Mabingwa.
Aidha, kiongozi wa Madaktari hao Dokta Peter Kyamba ametoa wito kwa wananchi wa Nachingwea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujipatia matibabu
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.