Leo, tarehe 19 Machi 2025, Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Nachingwea umefanyika katika ukumbi wa TTc Nachingwea, Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, aliongoza mkutano huu na kusisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta mshikamano kati ya walimu na kushirikiana na serikali.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Moyo amesisitiza kuwa madeni ya walimu ni jambo la msingi linalohitaji kutatuliwa haraka, pia alisema, "madeni sio suala la ihali, ni lazima walipwe, kwani bila kulipwa kwa wakati, morali ya walimu itashuka na ufaulu utaathirika", kunanahitajika bajeti maalum kwa ajili ya kulipa madeni na kuhakikisha posho na fedha za kujikimu zinatolewa kwa wakati.
Aidha, amesema kuwa serikali itakuja na mpango mahususi wa ujenzi wa nyumba za walimu ili kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya walimu, amesisitiza kwamba kuna uhaba wa walimu katika wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.