Tarehe 4 March ,Kikao cha Kamati ya Lishe Wilaya kimefanyika kwa mafanikio, kikizingatia robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025 (Oktoba - Desemba). Idara ya Afya kupitia kitengo cha Lishe, lengo likiwa ni kubadili mitazamo potofu kuhusu lishe na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kula chakula bora kwa afya.
Mhe.Mohamed Hassan Moyo amesisitiza kuwa Unga wenye virutubishi haipunguzi nguvu za kiume kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, bali inaboresha afya za watoto na jamii kwa ujumla. Amehimiza kila mmoja kuchukua jukumu la kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora, ili kuondoa mifumo ya upotoshaji.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Dkt. Ramadhani Mahiga, aliwataka wajumbe wa kikao na viongozi wa jamii kuongeza juhudi katika kusambaza elimu ya lishe bora, hasa kwa watoto. Alisisitiza kuwa elimu ni msingi muhimu wa kuboresha afya na maisha ya jamii, na aliwahimiza viongozi wa chini kuendelea kutoa mwongozo na msaada wa elimu kuhusu lishe bora.
Wajumbe walieleza umuhimu wa kuongeza mashine za kusaga virutubishi katika shule za msingi na sekondari, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula chenye virutubishi muhimu kwa ukuaji wao na afya bora.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.