Leo, Januari 7, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Mohamed Hassan Moyo, amekabidhi vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama "Machinga" katika kata ya Naipanga. Mhe. Moyo amewapongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kufanikisha zoezi hilo na kuhimiza wafanyabiashara kujitokeza mapema ili kuepuka kupitwa na fursa. Alisisitiza kuwa vitambulisho vya biashara vitawawezesha kutambulika na mamlaka kama TRA, Jeshi la Polisi, na kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea. Adnan Mpyagila, alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatambua wafanyabiashara hao na kuongeza mchango wao katika Pato la Taifa.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Bi. Stella Kategile, alieleza kuwa vitambulisho vitawawezesha wafanyabiashara kupata maeneo maalumu ya biashara na kutambulika kisheria.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.