Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo leo Agosti 16, 2024 amekabidhi mashine mpya ya kisasa ya kuchakata na kuthaminisha mbao kwa Umoja wa Vijiji vinavyohifadhi ya Misitu (UVIHIMINACHI)
Mhe. Moyo amewataka wataalamu wa Maliasili na Vjiji wanachama wa Umoja huo kuhakikisha mtambo huo unaleta matokeo chanya katika shughuli za uvunaji misitu kwa manufaa ya wananchi pamoja na kuhakikisha wanautunza kwa uangalifu wa hali ya juu.
Kwa upande wake Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ndugu Paiton Kamnana amesema mtambo huo utakwenda kuleta tija katika uvunaji kwani utaokoa muda, utazalisha mbao nyingi kwa muda mfupi na utawezesha kutoa huduma kwa wateja wengi, hivyo uvunaji utakua fanisi na wenye tija.
Aidha, Mwenyekiti wa Umoja huo ndugu Haji Mwembe amemshukuru Mkuu wa Wilaya na Serikali kwa ujumla kwa kuunga mkono shughuli za uvunaji misitu kwani zinaleta maendeleo kwa jamii, vipo vijiji vimeweza kutekeleza miradi kutokana na fedha za uvunaji mositu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.