ZOEZI LA KUWAONDOA TEMBO KUANZA DESEMBA 1, 2022 WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI
Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea Ndugu Omari S. Mwanga akiwa anamwakilisha Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Hashim A. Komba ameeleza kuanzia Tarehe 1, Desemba 2022 zoezi la kuwaondoa Tembo katika makazi na mashamba ya watu linatarajiwa kuanza rasmi. Katibu Tawala ameyasema hayo leo Novemba 28, 2022 Katika kikao kilichofanyika kata ya kipara kikiwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya kata zote zenye changamoto kubwa ya Tembo kama vile Mkoka, Namapwia, Ngunichile, Mnero Miembeni, Kilimarondo na Mbondo.
Mwanga, ameeleza jitihada za serikali katika kutatua changamoto ya Tembo kwa wananchi ilianza kwa kutoa elimu iliyohusisha njia mbalimbali za kuwaondoa Tembo katika maeneo ya makazi na mashambani, baadhi ya njia hizo pamoja na njia ya Oil chafu, Njia ya Pilipili, na Nyuki .
Wakati njia hizo zinaendelea kutumika ameeleza kuwa Tanzania Wildlife Management Authority ( TAWA ) kwakushirikiana na Tanzania Wildlife Research Institute ( TAWARI ) waliendelea na uchunguzi wa kubaini mtawanyiko wa Tembo na njia ambayo itatumika kuwapitisha Tembo wakati wa kuwaswaga au kuwaondoa kuwarudiaha eneo la hifadhi kwakutumia Helikopta.
Hatua ya kubaini mtawanyiko wa Tembo umeshakamilika hivyo, Desemba 1, 2022 zoezi la kuanza kuwaondoa Tembo litaanza mara moja kwa kutumia Helikopta. Ameeleza Katibu Tawala Omari S. Mwanga.
Aidha, katibu wala, ametumia fursa hiyo kuwasihii viongozi wa ngazi ya kata zote kwenda kutoa Taarifa kwa wananchi juu ya kuanza kwa zoezi hilo ambalo linafanyika Kati ya siku 5 Hadi 7 hivyo wananchi wanapaswa kuepuka matembezi yasiyo na ulazima hasa nyakati za usiku na kuwa watulivu wakati Helikopta itakavyokuwa inazunguka . Kufanikisha zoezi hilo linahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi .
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza kata ya Mkoka na kufuata kata zingine Kama vile Mnero Ngongo, Namapwia Nditi, Ngunichile kuelekea upande wa hifadhi ya Selous .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.