Feb 11,2025 Benki ya Taifa tawi la Mtwara kupitia Meneja wake bwana Melchiades Rutayebesibwa imetoa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea juu ya utambuzi wa Noti sahihi za Tanzania.
Akitoa mafunzo Bwana Rutayebesibwa ameeleza njia ambazo hutumika kutambua noti bandia na noti halali ikiwa ni pamoja utumiaji wa tochi maalumu ambazo hutumika kuchunguza alama elekezi zinazopatikana katika noti hizo.
Katika hatua nyingine Bw Rutayebesibwa ameeleza kuwa kazi ya benki hiyo ni pamoja na kuratibu masuala ya ubadilishaji wa fedha za kigeni na kuwataka wananchi kuripoti majanga mbalimbali ambayo hupelekea note hizo kuharibika ikiwa ni kufuata hatua zitakazomsaidia kuthibitisha majanga hayo na benki itamsaidia mripoti kulingana na maelezo husika.
Aidha Bw Cletus Mwakalinga ambae ni Meneja msaidizi wa benki hiyo ameeleza kuwa benki kuu imeondoa fedha zote za zamani kutokana na tangazo la Oct 2024 na kueleza kuwa kuanzia January mpka april 2025 wananchi wanatakiwa kubadilsha katika benki zilizopo karibu yao na badala yake hazitotumika tena.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Chionda Kawawa amewashukuru wakufunzi hao na kuwatakia majukumu mema katika kutoa elimu hiyo maeneo mengine na kuwataka kuendelea kutoa elimu hiyo mara kwa mara kwa lengo la kuongeza uelewa kwa wananchi
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.