Baraza la waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Nachingwea lapitia taarifa ya ufungaji wa hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kwa mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni 2023. Waheshimiwa madiwani wakiongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Adinani Mpyagila sambamba na Katibu wake kaimu Mkurugenzi Ndugu Lington Nzunda wakiongoza kikao hicho Cha kisheria kwa mujibu wa kifungu Na 43 Cha sheria ya fedha za serikali za mitaa sura 290 (The Local Government Finance Act ), agizo katika kanuni za fedha za serikali za Mitaa Na 31 (The Local Authority Financial Memorandum of 2009 ) pamoja na vifungu vyake zinaelekeza Halmashauri zote kuandaa taarifa ya fedha za mwisho wa mwaka (Annual Statements ) na kuziwasilisha kwa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kabla au ifikapo Tarehe 30 Septemba ya kila mwaka .Hivyo kwa kuzingatia utaratibu huo Baraza limepitia taarifa kuu tatu zinazojumuishwa kwenye taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka ambazo kisheria na kikanuni zinatakiwa ziidhinishwe kabla ya kukaguliwa na CAG ambazo ni
Mizani (Statement of financial Position ) ambapo inaonesha Mali zinazomilikiwa na Halmashauri pamoja na madeni inayodaiwa hadi kufikia 30 Juni 2023 . Hadi kufika Juni 30, 2023 Halmashauri ilikuwa na Mali zenye thamani ya Sh Bilioni 55.718,
Kwa upande wa Taarifa ya Mapato na Matumizi (Statement of financial Performance ) hadi kufikia Juni 30, 2023 Halmashauri ilipokea jumla ya Tzs Bilioni 35.702 kutoka katika vyanzo mbalimbali ambapo mapato yameongezeka kwa TZS Bilioni 3.459 na upande wa matumizi halmashauri ilitumia jumla Sh Bilioni 29.317 hadi kufikia Tarehe 30 Juni 2023 .Na Taarifa ya Mtiririko wa fedha Taslimu ( Cash Flow Statement ) .
Hii inaonesha mwenendo wa mapokezi ya fedha Taslimu kwa mwaka mzima kutoka katika vyanzo mbalimbali ambapo Jumla ya TZS Bilioni 35. 542 zilionekana kupokelewa ambapo Bilioni 29.546 zilitumika katika shughuli za kawaida na kiasi Cha TZS Bilioni 1.913 zilitumika katika shughuli za uwekezaji . Mwisho wa mwaka wa fedha Halmashauri ilibakiwa na jumla ya fedha TZS Bilioni 4.083 kwenye akaunti mbalimbali .Waheshimiwa baada ya kupitia taarifa hizo wameridhishwa na kupongeza kwa matumizi sahihi.
#tukovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.