Akina mama wilayani Nachingwea wameonyesha furaha na kuthamini mafunzo waliyopata kuhusu unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika leo Agosti, 7 2025, katika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea.
Katika maadhimisho hayo, ambayo hufanyika kila mwaka kati ya tarehe 1 hadi 7 Agosti duniani kote, washiriki wamepata elimu ya kina kuhusu mbinu sahihi za unyonyeshaji, umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto katika miezi sita ya mwanzo bila kuongeza chakula kingine, pamoja na njia bora za kuandaa lishe endelevu kwa watoto waliofikia miezi sita na kuendelea,
Akizungumza katika hafla hiyo, Irene Benjamin ambae ni Afisa lishe wa Halmashauri ya wilaya nachingwea, amesema kuwa elimu inayotolewa inalenga kuhakikisha akina mama wanakuwa na uelewa sahihi wa afya ya mtoto, hususan katika hatua za awali za malezi ya mtoto
Aidha, akina mama walioudhuria maadhimisho hayo wanaishukuru serikali kwa kuandaa siku maalum za kuelimisha jamii juu ya masuala ya lishe na unyonyeshaji, kupitia elimu hiyo wameweza kujifunza namna kina baba wanavyoweza kuwasaidia kulea watoto kwa njia bora,
Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani hutoa fursa kwa jamii kupata elimu kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu umuhimu wa maziwa ya mama, huku maafisa lishe wakisisitiza jukumu la kina Baba kuwasapoti wake zao katika suala zima la kulea watoto kwa pamoja.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.